Monday, 4 May 2015

THE BEREANS SDA CHURCH CHOIR - CHANUKA

Zamani nilipokuwa motto,nilifikiria kama mtoto,nilisemasema kama mtoto niliyoyatenda ni ya utoto,sirudi nyuma nimekuwa mzima maisha mapya ndani ya yesu  x2
                                                                                CHORUS
                Chanuka ndani yake yesu,Vuka utoto wa kiroho Imarika kwa msingi wa neno,chakula bora cha kiroho,piga hatua songa mbele,mpaka lini u motto,komaa,usherehekee maisha mapya ndani ya yesu  x2

Zamani nilipokuwa motto,nilikula chakula cha mtoto,nilibembelezwa kama mtoto,nililialia kama mtoto,sirudi nyuma nimekuwa mzima,maisha mapya ndani ya Yesu (Christo)  x2

                                                    Kusoma neno kwako balaa (dalili ya utoto wa kiroho)
                                                    Zaka nasadaka kabisa hutoi(dalili ya utoto wa kiroho)
                                                    Wakati wa shida ndio waomba(dalili ya utoto wa kiroho)
                                                    Upendo wa mdomo bila matendo(dalili ya utoto wa kiroho)
                                                    Ukabila na siasa hata kanisani jamani(dalili ya utoto wa kiroho)
                                                    Kigeugeu kama kinyonga(dalili ya utoto wa kiroho)
                                                             
                                                                       (CHORUS) X3

                                             Chanuka ndani yake yesu,Vuka utoto wa kiroho Imarika kwa msingi wa   neno,chakula bora cha kiroho,piga hatua songa mbele,mpaka lini u motto,komaa,usherehekee maisha mapya ndani ya yesu  x2

THE BEREANS SDA CHURCH CHOIR - AMKA ACHA USINGIZI

Amka acha usingizi wa dhambi pambazuko ni karibu (asema) Bwana aaaa(Yesu),kwani yajayo huwezi yajua sasa amka naye Bwana Yesu

                                                    CHORUS
                        Wengi wanajivunia kwamba wao wamja Mungu,lakini matendo yao ni ya asili ya dhambi,(wajichunguze,wagutuke wasilale asubuhi kumepambazuka x2)x2

Kesha ukiomba ndugu uwe macho pambazuko ni karibu (asema) Bwana aaaa (Yesu), tubu dhambi zako uhesabiwe haki hujui mwisho wako ndugu  x2

                                                                CHORUS

Wengi wanajivunia kwamba wao wamja Mungu,lakini matendo yao ni ya asili    ya dhambi,(wajichunguze,wagutuke wasilale asubuhi kumepambazuka x2)x2

email--------------eastgospel@gmail.com

THE BEREANS SDA CHURCH CHOIR - ALITEMBEA

Alitembea kwa ujasiri ili afikie uponyaji,alikaza mwendo na kufika pale alipokuwa mkombozi Yesu,aligusa pinde la nguo yake ndipo akapata kupona.  X2

                                                                CHORUS
Imani yake kwake Mwokozi haikuwa ya kusitasita alikazana kufika pale mwisho akakuwa    huru uu,nawe mwenzangu una nafasi, harakisha ungali na muda, ukiwa nayo imani kwake mwisho utakuwa huru  x2

Nawe tembea kwa ujasiri uje kwake Bwana mponyaji, shida zako zote anazitambua leta zote kwake mkombozi yesu,ataondoa zote na kuweka huru mwisho utapata kupona.

                                                         CHORUS

Imani yake kwake Mwokozi haikuwa ya kusitasita alikazana kufika pale mwisho akakuwa    huru uu,nawe mwenzangu una nafasi, harakisha ungali na muda, ukiwa nayo imani kwake mwisho utakuwa huru  x2

 email......eastgospel@gmail.com